Watu 10 wauawa katika shambulizi nchini Cameroon
2023-07-18 08:36:22| cri

Wizara ya Ulinzi ya Cameroon imesema, watu 10 wameuawa na wengine wawili kujeruhiwa vibaya katika shambulio lililotokea jumapili huko Bamenda, mji mkuu wa Mkoa wa Kaskazini-Magharibi wa eneo linalozungumza Kiingereza.

Taarifa hiyo imesema saa 1:30 jioni kwa saa za huko, zaidi ya wapiganaji kumi waliwafyatulia risasi watu karibu na baa moja huko Bamenda, na kuua watu 10, wakiwemo wanawake, na kuongeza kuwa, idara za usalama zinaendelea kuwasaka washambuliaji hao.