Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) jana imeahidi kuiunga mkono Zambia baada ya nchi hiyo kufikia makubaliano na wadeni wake rasmi juu ya kupanga upya utaratibu wa madeni.
Akizungumza alipokutana na rais wa Zambia Hakainde Hichilema mjini Lusaka, rais wa Benki hiyo Akinwumi Adesina amesema, Benki yake inafikiria machaguo mbalimbali katika kuiunga mkono Zambia, ikiwemo kuboresha uwezo wa nchi hiyo wa kujadili madeni yake kufuatia mchakato wa upangaji mpya wa madeni hayo.
Kwa upande wake, rais Hichilema ameishkuru AfDB kwa kuiunga mkono, na kutoa wito kwa msaada zaidi kufuatia nchi hiyo kuingia kwenye awamu ya majadiliano na wadeni wake kutoka sekta binafsi.