Soko la matumizi la China larejea hatua kwa hatua kwenye hali ya kawaida
2023-07-19 21:07:29| cri

Mkurugenzi wa wizara ya biashara ya China tarehe 18 alisema soko la matumizi la China linarejea hatua kwa hatua kwenye hali ya kawaida.

Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, thamani ya jumla ya biashara ya rejareja ya bidhaa za matumizi nchini China imefikia yuan trilioni 22.76 (sawa na dola trilioni 3.17 za kimarekani), kiasi ambacho kimeongezeka kwa aslimia 8.2 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hicho. Thamani ya biashara ya rejareja mtandaoni imefikia yuan trilioni 7.16 (sawa na dola trilioni moja za kimarekani), kiasi ambacho kimeongezeka kwa asilimia 13.1 ikilinganishwa na mwaka jana.