Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameonya kwamba dunia imeacha njia ya kufikia malengo ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030, na kutoa wito kwa nchi kufanya mabadiliko katika mwaka huu na kuongeza hatua sasa.
Bw. Guterres amesema, hivi sasa utekelezaji wa zaidi ya nusu ya malengo ya maendeleo endelevu ni dhaifu, na karibu theluthi moja ya malengo yamedumaa hata kurudi nyuma.
Pia amesisitiza kuwa, nchi zilizoendelea zinapaswa kutimiza ahadi zao kuhusu ufadhili wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, ikiwa ni pamoja na kutoa dola za kimarekani bilioni 100 zilizoahidiwa mwaka huu.