Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bi. Mao Ning amesema, kutokana na hali ya sasa ya Sudan, serikali ya China itatoa msaada wa dharura wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 1.4 kwa nchi hiyo, ili kupunguza mgogoro wa kibinadamu nchini humo.
Bi. Mao Ning amesema, China itaendelea kutoa msaada wa kibinadamu kwa Sudan kwa mujibu wa mahitaji ya nchi hiyo, na kuisaidia kukabiliana na mgogoro huo wa kibinadamu.
Bi. Mao amesema, jumamosi iliyopita, vifaa vya matibabu vilisafirishwa kwenda Sudan, na tani mia 9 za msaada wa chakula zinatarajia kusafirishwa katikati ya mwezi Agosti.