Shirika la fedha la Kimataifa IMF limeidhinisha msaada wa Kuongeza Mikopo wa dola milioni 271 kwa Burundi, ambapo zaidi ya dola milioni 62 zikiwa za kwanza kutolewa mara moja.
Uchumi wa nchi hiyo ndio kwanza unaanza kuimarika kutokana na mzozo wa miaka mingi na misukosuko ya kisiasa ambayo iliacha sekta kuu zikiwa na dosari.
IMF ilisema mkopo huo utasaidia kusaidia ajenda ya mageuzi ya serikali. Mageuzi ya kiuchumi yameanza kufanikisha sekta muhimu za kiuchumi huku wanauchumi wengi wakitarajia nchi hiyo kuinuka haraka kiuchumi.