Rais wa China afanya mazungumzo na mwenzake wa Algeria
2023-07-19 08:41:00| CRI

Rais Xi Jinping wa China jana amefanya mazungumzo na rais Abdelmadjid Tebboune wa Algeria ambaye yupo ziarani nchini China.

Katika mazungumzo hayo, rais Xi amesisitiza kuwa, China inapenda kushirikiana na Algeria kutekeleza matokeo yaliyofikiwa kwenye Mkutano wa Kwanza wa Kilele wa China na nchi za Kiarabu, kutekeleza kihalisi Hatua Nane za Pamoja za ushirikiano kati ya pande hizo mbili, kuimarisha ushirikiano chini ya mfumo wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), na kutekeleza kikamilifu matokeo yaliyopatikana katika Mkutano wa Dakar wa baraza hilo, ili kuhimiza ujenzi wa Jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya China na Algeria, na China na Afrika katika zama mpya.

Kwa upande wake rais Tebboune amesema Algeria inapenda kujiunga na ujenzi wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, kukuza uhusiano wa kiwenzi na kimkakati kwa pande zote kati ya nchi hizo mbili, ili kusaidia Algeria kupata maendeleo ya uchumi na jamii.