Rais Xi Jinping akutana na aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Henry Kissinger
2023-07-20 15:57:14| cri

Rais Xi Jinping wa China leo hapa Beijing amekutana na aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Henry Kissinger ambaye yuko ziarani nchini China.

Rais Xi amebainisha kuwa Dkt. Kissinger ambaye ametimiza umri wa miaka 100, amefanya ziara zaidi ya 100 nchini China. 100 hizo mbili zikiwekwa pamoja, zimeipa ziara hii umuhimu maalum. Katika miaka 52 iliyopita, mwenyekiti hayati Mao Zedong, aliyekuwa rais wa Marekani Richard Nixon na Dkt. Kissinger mwenyewe, walifanya uamuzi sahihi wa kuanzisha mchakato wa kurejesha uhusiano wa nchi hizo mbili kwenye hali ya kawaida, uamuzi ambao si kama tu umenufaisha nchi hizo mbili, na bali pia umenufaisha dunia nzima. Rais Xi amesema, kamwe wachina hawawezi kumsahau rafiki wao mkubwa, na kamwe hawatasahau mchango wa Dkt. Kissinger katika kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano na urafiki kati ya China na Marekani.

Kwa upande wake Dkt. Kissinger amesema ni fahari kwake kuweza kuitembelea China, na pia anaishukuru China kwa kupanga mkutano huo kwenye jengo la No. 5 katika Jumba la Wageni wa Taifa la Diaoyutai, ambako alikutana kwa mara ya kwanza na viongozi wa China. Dkt. Kissinger amesisitiza kuwa, uhusiano kati ya Marekani na China unahusiana na amani ya dunia na maendeleo ya jamii ya binadamu.