Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mkondo wa El Nino unatarajiwa kuwepo katika kipindi cha mvua za msimu wa vuli zitakazoanza kunyesha Oktoba hadi Desemba mwaka huu, na kuathiri maeneo mbalimbali ya Tanzania.
Meneja wa Utabiri wa hali ya hewa wa TMA Dk Mafuru Kantamla, amesema hadi sasa inaonyesha kuna uwezekano wa asilimia 90 ya kuwepo kwa El Nino hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu. Ameyataja maeneo ambayo yataathirika na mvua za El nino kuwa ni mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Lindi na Mtwara.
Lakini pia amesema El Nino haitaathiri pwani ya bahari ya Hindi pekee, kwani itasambaa hadi katika maeneo ya nyanda za juu Kaskazini na ukanda wa Pwani.