Jeshi la Sudan jana limetoa taarifa likisema, watu 14 wameuawa na wengine 15 kujeruhiwa katika shambulizi la ndege zisizo na rubani lililofanywa na Vikosi vya Msaada wa Dharura (RSF) huko Khartoum, mji mkuu wa nchi hiyo.
Taarifa hiyo imesema, vikosi vya RSF vilitumia ndege zisizo na rubani kushambulia watu waliokuwa wakiwapokea askari wa jeshi la Sudan kwenye eneo la Al-Azouzab.
Jeshi la Sudan limesema litaendelea kufanya msako katika maeneo ya vituo vya RSF mjini Khartoum.