Uwekezaji wa kigeni kwenye sekta zinazofungamana na uchimbaji na usambazaji wa mafuta nchini Uganda umeongezeka na kufikia trilioni 5.5 za Uganda. Kwa mjibu wa shirika la biashara la umoja wa mataufa UNCTAD, uwekezaji wa kigeni kwenye sekta ya kawi uliongezeka kutoka shilingi trilioni1.5 mwaka wa 2021 hadi shilingi trilioni 5.5 mwaka wa 2022.
China kupitia kwa kampuni ya China National Offshore Oil cooperation CNOOC ilikiwekeza dola bilioni 6.5 kwenye sekta ya kawi. Huku makampuni mengine ya kigeni yakiwekeza trilioni 12.8 kwenye mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta lenye urefu wa kilomita 1,440 kutoka Tanga Tanzania hadi visima vya mafuta vya Albert nchini Uganda.
Japo uwekezaji huo umeongezeka, mamlaka ya uwekezaji ya Uganda UIA imesema kiwango hicho bado ni cha chini ikilinganishwa na matarajio na malengo ya nchi. UIA inasema inatarajia uwekezaji wa angalau trilioni 10.93 hadi trilioni 14.57 kila mwaka ili kupanua uchumi wake pamoja na kuongeza nafasi za ajira.