Kampuni ya utoaji huduma za intanenti ya Starlink yafika Kenya
2023-07-20 10:01:52| cri

Kampuni ya utoaji huduma za intanenti ya

inayomilikiwa na Elon Musk ambaye pia ni mmiliki wa jukwa la mawasiliano la Twitter imeingie Kenya. Starlink inatarajiwa kushindana na kampuni kama vile Zuku, Jamii Telekom na Safaricom katika utoaji wa huduma za data. 

Starlink tayari imeafikia makubaliano na kampuni ya Karibu Connect kuuza vifurushi vya data kote nchini. Wakati huo huo Safaricom, ambayo hivi sasa inaongoza katika utoaji wa huduma za data na mawasiliano nchini Kenya imesaini makubaliano na kampuni AST SpaceMobile kusambaza data kwa mfumo wa setilaiti kama unaotumiwa na Starlink lengo kuu likiwa kufikia maeneo ambayo yamesalia nyuma katika kupokea huduma za data.