Kundi la 43 la jeshi la majini la China limehitimisha ziara yake ya kirafiki nchini Jamhuri ya Kongo jumanne wiki hii na kuondoka katika Bandari ya Pointe-Noire saa nne asubuhi kwa saa za huko, ikiashiria kukamilika kwa mafanikio kwa majukumu ya kikosi cha 43 cha jeshi la majini la China kutembelea nchi tano za Afrika Magharibi.
Wanajeshi wa pande hizo mbili walifanya mazoezi na uratibu wa pamoja, pamoja na mafunzo ya jinsi ya kupambana na ugaidi na mbinu za kupambana na uharamia.
Aidha, kikosi cha matibabu cha kundi hilo la China na kikosi cha 29 cha Madaktari wa China walifanya kliniki ya pamoja ya bure katika Hospitali ya De Loandjili mkoani Pointe-Noire, na kufanya mazungumzo ya kina na madaktari kutoka Hospitali Kuu ya Jeshi la Kongo na Hospitali ya De Loandjili juu ya kinga na matibabu ya magonjwa ya kawaida.