Wataalamu wasema mafunzo ya China kuondokana na umasikini ni muhimu kwa Afrika
2023-07-21 08:43:53| CRI

Wataalamu wamesema nchi za Afrika zinaweza kujifunza kutokana na mafanikio makubwa ya kampeni ya China ya kuondokana na umasikini uliokithiri ili kuendeleza maendeleo yao.

Wataalamu hao wamesema hayo jumatano wiki hii katika semina iliyofanyika kwa njia ya mtandao iliyoandaliwa kwa pamoja na Ubalozi wa China nchini Rwanda na gazeti la Africa-China Review la nchini Rwanda linalojikita katika ushirikiano kati ya China na Afrika.

Mtafiti wa kimataifa kutoka nchini Kenya, Adhere Cavence amesema, mfumo uliotumika nchini China unaweza kufanya kazi barani Afrika, na kwamba nchi za Afrika zinaweza kujifunza kutokana na uzoefu wa China katika kuondokana na umasikini.

Mwanadiplomasia wa Rwanda Zeno Mutimura amesema, Afrika inaweza kuiga uzoefu wa China ili kupunguza umasikini katika bara hilo, ikiwemo sera ya kutoa kipaumbele kwa wananchi kwanza.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Peking, Xia Qingjie amesema, kanuni kuu ya mafanikio ya kiuchumi ya China ni pamoja na serikali yenye nguvu iliyojitolea kuhakikisha ustawi wa wananchi na kuwawezesha watu kupata elimu bora na huduma za afya.