Kongamano la pili la uvumbuzi wa vyombo vya habari duniani lafanyika Shanghai
2023-07-21 14:06:00| cri

Kongamano la pili la uvumbuzi wa vyombo vya habari duniani lililoandaliwa na Shirika kuu la utangazaji la China CMG na serikali ya Shanghai limefanyika mjini Shanghai, China. Kongamano hilo lenye kaulimbiu ya “Ufunguaji, Ushirikishi na Kunufaishana-Kushikana Mikono Kuelekea Ustawi wa Kisasa”, umehudhuriwa au kushirikiwa kwa njia ya mtandao na wajumbe kutoka sekta mbalimbali ikiwemo mashirika ya kimataifa, vyombo vikuu vya habari vya ndani na nje ya China, Majopo ya Washauri Bingwa na makampuni ya kuvuka mipaka.

Mkuu wa CMG Bw. Shen Haixiong amesema katika mpango unaotolewa chini ya pendekezo la maendeleo duniani (GDI), pendekezo la usalama duniani (GSI) na pendekezo la ustaarabu duniani (GCI) yaliyotolewa na rais Xi Jinping, kushikana mikono katika kusukuma mbele maendeleo ya mambo ya kisasa na ustaarabu wa binadamu ni jukumu la vyombo vya habari.

Amesema ni muhimu kutekeleza jukumu la vyombo vya habari, kusimulia vizuri ujenzi wa mambo ya kisasa. Baada ya kufungwa kwa mkutano mkuu wa 20 wa Chama cha CPC, CMG imefanya shughuli mbalimbali kote duniani ikiwemo “China iliyoko katika safari mpya na dunia”, “Usasa wa mtindo wa kichina na dunia”, ili kujadili thamani ya kizama ya usasa wa mtindo wa kichina na umuhimu wake kwa dunia .