Kampuni kubwa ya mawasiliano ya China, Huawei, imesema itaboresha ujuzi wa kidijitali kwa vijana nchini Kenya kupitia teknolojia ya 5G, na inatarajia kuwafikia vijana 1,200 itakapofika mwaka 2024.
Mratibu wa shughuli za kijamii wa kampuni hiyo tawi la Kenya, Ian Korir amesema, madarasa ya kuhamishika yanayotumia umeme wa jua, yameongeza nguvu ya mtandao wake kuwa ya 5G, kwa kuwa inalenga kuongeza idadi ya vijana wanaoweza kunufaika na mafunzo ya ujuzi wa kidijitali.
Amesema katika miaka mitatu na nusu iliyopita, madarasa hayo yalitoa mafunzo ya ujuzi wa teknolojia ya habari na mawasiliano (ICT) kwa zaidi ya vijana 3,000 katika kaunti 25 nchini Kenya.