Soko la hisa la Kenya lipata hasara ya dola milioni 141 kufuatia msururu wa maandamano yanayoendelea kulalamikia gharama ya juu ya maisha. Mashirika ya uchukuzi wa angani, makampuni ya mabasi, benki na maduka ya jumla ni baadhi ya biashara ambazo zimeripoti hasara kufuatia maandamano hayo.
Mashirika ya ndege ya nchini Kenya, ikiwa ni pamoja na Safarilink, yanasema idadi ya abiria imepungua kwa hadi asilimia 40 katika siku chache zilizopita, hali imekuwa sawiya kwenye sekta ya usafiri wa barabarani. Benki nyingi jijini Nairobi, Kisumu na Mombasa zilifunguwa huku wamiliki wa maduka ya jumla ambayo kwa siku za hivi karibuni yamekuwa yakivamiwa na bidhaa kuporwa na waanadamanaji yakiongeza ulinzi japo yalisalia kufungwa.
Soko la Hisa la Nairobi (NSE) Jumatano lilipoteza Shilingi bilioni 20.725 katika siku ya kwanza ya maandamano ya siku tatu yanayoendelea.