IOM yaunda mkakati wa kudumu wa kusaidia wakimbizi nchini Sudan Kusini
2023-07-21 08:42:46| cri

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limesema kuwa linaandaa mkakati wa suluhisho la kudumu ili kusaidia jamii zilizoathiriwa na wakimbizi katikati ya Sudan Kusini.

IOM imesema imeandaa mkutano wa siku mbili katika Kaunti ya Yei, jimbo la Equatoria ya Kati, ambayo inashuhudia idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani na wakimbizi, ambao utasaidia kutambua njia na hatua zinazoweza kusaidia suluhisho endelevu na la kudumu kwao katika eneo linalokabiliwa na uhaba wa rasilimali na kuongezeka kwa mgogoro katika udhibiti wa ardhi na utawala.