Watalaam wairai Uganda kuwekeza zaidi katika kilimo
2023-07-21 11:02:13| cri

Serikali ya Uganda imesema ipo haja ya kutathmini tena sera ya kilimo na kuipa sekta hiyo kipaumbele iwapo taifa hilo la Afrika mashariki linataka kukua kiuchumi. Akizungumza kwenye kongamano la wahasibu linaloendelea Entebbe, kiranja wa serikali ya Uganda Hamson Obua amesema  nchi hiyo inafaa kuboresha sera za kilimo na usindikaji wa bidhaa za kilimo iwapo inataka kujiendeleza kiuchumi ikizingatiwa kwamba kilimo ni uti wa mgongo wa Uganda.

Takwimu kutoka kwa ofisi ya kitaifa ya takwimu zinaonyesha kuwa sekta ya kilimo imewaajiri rai wasiopungua milioni 7.2  wengi wao wakiwa wale wanaojishughulisha upanzi wa vyakula.

Obua ameongeza kusema kuwa kuimarishwa kwa viwanda hasa vya kilimo ni mojawapo ya mabadiliko katika sera ya kilimo ambayo Uganda inapaswa kutekeleza ili kuafikia agenda yake ya mwaka 2040 ya utoshelevu wa chakula.