Mapato ya Ethio-Telecom yaongezeka kwa dola bilioni 1.38
2023-07-21 11:01:45| cri

Kampuni ya mawasiliano ya Ethio-Telecom inayomilikiwa na serikali ya Ethiopia imeripoti kuonngeza kwa pato lake la kila mwaka hadi dola bilioni 1.38 hili likiwa ongezeko la asilimia 23.5% ya mapato. 

Afisa mkuu mtendaji wa Ethio-Telecom amesema kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, kampuni hiyo imeshuhudia ukuaji thabiti  ambao umeiwezesha kutoa huduma na bidhaa 203 tofauti. 

Mafanikio hayo ya Ethio-Telecom yametokana na mikakati yake ya  kuanzisha teknolojia mpya, kupanua ufikiaji wa mtandao wa simu na kutoa huduma zinazowalenga wateja.

Kulingana na data ya kampuni hiyo, wateja wa Telebirr, huduma ya kifedha ya simu ya Ethio-Telecom iliyozinduliwa Mei 2021, wwamefika milioni 34.3 na wateja hawa wamefanya miamala yenye thamani ya birr bilioni 679.2 katika mwaka wa fedha wa 2022/2023.