China yazitaka pande husika zitatue suala la usalama wa chakula wa kimataifa kwa kupitia mazungumzo
2023-07-21 08:43:06| cri


 

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bi. Mao Ning jana amesema, China inazitaka pande husika zifanye mazungumzo na majadiliano ili kutatua vizuri suala la usalama wa chakua wa kimataifa.

Bi. Mao amesisitiza kuwa, msimamo wa China kuhusu mgogoro wa Ukraine siku zote ni wazi, na China pia itaendelea kuonesha umuhimu wa kiujenzi kwa kuhimiza utatuzi wa kisiasa wa mgogoro huo.

Awali, Russia iliyojitoa kwenye makubaliano ya usafirishaji wa chakula kupitia Bahari Nyeusi, ilitangaza kuwa meli yoyote ya uchukuzi inayokwenda Ukraine kupitia Bahari hiyo itachukuliwa kuwa na malengo ya kijeshi.