Jeshi la Sudan limesema watu tisa wamefariki katika ajali ya ndege ya abiria iliyotokea jana kwenye uwanja wa ndege wa Bandari ya Sudan katika Jimbo la Bahari Nyekundu, mashariki mwa nchi hiyo.
Taarifa iliyotolewa na Jeshi hilo imesema, ajali hiyo ilitokea baada ya ndege hiyo kuanguka kutokana na hitilafu za kiufundi wakati inapaa.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, watu tisa waliouawa ni pamoja na wanajeshi wanne, lakini msichana mmoja alinusurika kwenye ajali hiyo.