Rais wa China kuhudhuria ufunguzi wa Michezo ya 31 ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Duniani ya Majira ya Joto mjini Chengdu
2023-07-24 10:34:46| cri

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Hua Chunying amesema, rais Xi Jinping Julai 27 hadi 28 atahudhuria hafla ya ufunguzi wa Michezo ya 31 ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Duniani ya Majira ya joto mjini Chengdu, na kufanya karamu ya kuwakaribisha viongozi wa nchi za nje watakahudhuria hafla hiyo na kufanya ziara nchini China.

Viongozi wa nchi za nje watakaohudhuria hafla hiyo ni pamoja na rais Joko Widodo wa Indonesia, rais Mohamed Ould Cheikh Al Ghazouani wa Mauritania, rais Évariste Ndayishimiye wa Burundi, rais Irfaan Ali wa Guyana, waziri mkuu wa Georgia Irakli Garibashvili, na waziri mkuu wa Fiji Sitiveni Rabuka.