Waziri Mkuu wa Tanzania ataja faida za mafunzo ya IAWP kwa askari wanawake
2023-07-24 10:35:22| cri

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kuna faida ambazo nchi hiyo itazipata kupitia Mafunzo ya Kimataifa ya Askari Wanawake wa Ukanda wa Afrika (IAWP).

Bw. Majaliwa amesema hayo kwenye ufunguzi wa Mafunzo ya Kimataifa ya Askari Wanawake kanda ya Afrika (IAWP), uliofanyika jana jumapili jijini Dar es Salaam. Amesema mafunzo hayo yatawajengea uwezo askari wanawake na kuwawezesha kubadilishana uwezo na uzoefu kutoka nchi mbalimbali zikiwemo Afrika Kusini, Botswana, Ethiopia na Zimbabwe.

Pia amesema kuna fursa ya kujifunza utamaduni ili kuimarisha uhusiano ambao kimsingi askari watapata maarifa katika utendaji wao wa kila siku.