Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) mkoa wa Ituri, Jules Ngongo, amesema, askari wa jeshi hilo amewaua watu 13 kuanzia Jumamosi hadi Jumapili kwenye kijiji cha Nyamamba mkoani humo.
Ngongo amesema, wengi waliouawa ni ndugu wa askari huyo, wakiwemo watoto kumi, na kuongeza kuwa, chanzo cha shambulio hilo ni mgogoro wa kifamilia.
Mamlaka za kijeshi zimeunda tume ya upepelezi kufanya uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo.