Mashindano ya soka ya ngazi ya vijiji mkoani Xinjiang
2023-07-24 07:53:26| CRI

Katika siku za karibuni, mashindano ya soka ya Kombe la Umoja huko Kashi, katika mkoa unaojiendesha wa Xinjiang sio tu yamekuwa yanajulikana nje ya mkoa huo, bali pia yamemvutia mwanahabari kutoka Afrika kuja kuyatazama. Washiriki wa Kombe hili ni wachezaji wa ridhaa, pia ni wanakijiji wa kawaida wa makabila mbalimbali kutoka vijiji na vitongoji zaidi ya 160. Miongoni mwao, wengi hawajawahi kupewa mafunzo maalum, lakini wameonyesha uwezo mkubwa wa kucheza soka na moyo wa umoja. Je, kwanini kumeibuka mashindano ya soka ya ngazi ya vijiji kama haya? Hebu tujiunge na mwanahabari Fadhili Mpunji kutoka Tanzania huko Kashi.