Watu 12 wafariki baada ya jengo kuanguka nchini Cameroon
2023-07-24 07:54:02| CRI

Watu 12 wamefariki na wengine 19 kujeruhiwa baada ya jengo la ghorofa nne kuanguka kwenye eneo la kibiashara la Douala, nchini Cameroon, mapema jana.

Gavana wa mkoa wa Littoral Ivaha Diboua amesema, kati ya watu waliofariki ni wanawake na watoto, na kuongeza kuwa, kazi ya uokoaji bado inaendelea kuwatafuta watu waliokwama kwenye kifusi.

Amesema jeshi, kikosi cha zimamoto, polisi na vikosi vyote vya usalama vinashirikishwa katika kazi ya uokoaji, na kwamba huenda idadi ya watu waliofariki ikaongezeka.