Wizara ya Mambo ya Ndani ya Algeria imesema, idadi ya watu waliofariki kutokana na moto wa porini kaskazini mwa nchi hiyo imeongezeka na kufikia 34, wakiwemo wanajeshi 10. Wizara hiyo imesema, watu 8,000 wanakabiliana na moto huo katika mikoa 11, wakisaidiwa na malori 529 na helikopta kadhaa za kikosi cha zima moto.