Serikali ya mkoa wa Heilongjiang yachunguza kikamilifu ajali ya kuanguka kwa paa la ukumbi wa michezo mjini Qiqihar
2023-07-25 08:21:32| cri

Ofisi ya habari ya serikali ya mji wa Qiqihar nchini China imetoa ufafanuzi halisi kuhusu ajali ya kuanguka kwa paa la ukumbi wa michezo katika Shule ya Sekondari Namba 34 katika mji huo.

Kwa mujibu wa Meya wa mji huo Bw. Shen Hongyu, watu 11 walifariki katika ajali hiyo iliyotokea jumapili iliyopita, wakiwemo walimu na wanafunzi.

Serikali ya mkoa wa Heilongjiang imeunda timu ya pamoja ya uchunguzi, ambayo itachunguza kwa kina kujua chanzo cha ajali hiyo, na kuwajibisha wahusika kwa mujibu wa sheria.