Mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Bw. Wang Yi, jana alifanya mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Afrika Kusini Bi. Naledi Pandor mjini Johannesburg.
Wang Yi amesema, mfumo wa BRICS ni jukwaa muhimu zaidi kwa wawakilishi wa masoko mapya yanayoibuka na nchi kubwa zinazoendelea ili kuimarisha majadiliano na ushirikiano, na pia ni njia muhimu zaidi kwa nchi za Kusini na Kusini kufanya mawasiliano ya kimkakati. Amesema China inaiunga mkono Afrika Kusini ambayo ni nchi mwenyekiti wa BRICS na mwenyeji wa mkutano wa 15 wa viongozi wa BRICS, kupokea maombi ya nchi husika kushiriki kwenye ushirikiano wa BRICS, kuhimiza maendeleo na kupaza zaidi sauti ya BRICS, kulinda haki na usawa wa kimataifa, kutekeleza ushirikiano wa pande nyingi, na kuleta utulivu katika dunia ya sasa iliyoko katika hali ya taharuki na sintofahamu.
Bi. Pandor amesema, Afrika Kusini inapenda kuongeza mawasiliano na China na nchi nyingine za BRICS ili kufanikisha mkutano huo na kuhimiza ushirikiano wa BRICS ufikie katika ngazi ya juu zaidi.