UM wasema mapigano nchini Sudan yamesababisha vifo na majeruhi na kwa maelfu ya raia wa nchi hiyo
2023-07-25 10:26:36| cri

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia Masuala ya Kibinadamu (OCHA) limesema, mapigano nchini Sudan yamesababisha vifo na majeruhi kwa maelfu ya raia wa nchi hiyo, na mamilioni wengine kukimbia makazi yao.

Ofisi hiyo imesema, mapigano hayo yaliyodumu kwa siku 100 sasa yamesababisha madhara makubwa kwa raia, na yanapaswa kusimamishwa sasa.

Ofisi hiyo pia imesema, Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limeripoti kuwa, katika kipindi hicho, mtoto mmoja anajeruhiwa ama kuuawa katika kila saa ya mapigano hayo. Takwimu hizo zinatokana na ripoti halisi inayosema kuwa, watoto 435 wameuawa na wengine Zaidi ya 2,000 kujeruhiwa katika siku 100 zilizopita.

Ofisi hiyo imesema, ripoti iliyotolewa na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) imezingatia ongezeko la kasi la watu wanaokimbilia nchi jirani kukwepa mapigano nchini Sudan.