Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, leo ataweka jiwe la msingi la ujenzo wa mnara mpya wa kumbukumbu ya mashujaa katika mji mkuu wa nchi hiyo, Dodoma, kama sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa nchini humo.
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Masuala ya Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama, amewaambia wanahabari mjini Dar es Salaam kuwa, mnara huo utatumika kama sehemu ya kumbukumbu kwa askari waliojitolea maisha yao kupigania nchi yao.
Amesema shughuli za kuadhimisha siku hiyo ni pamoja na viongozi kuweka mashada ya maua katika kuwakumbuka mashujaa hao.
Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa nchini Tanzania huadhimishwa kila Julai 25.