Rais Xi asisitiza usimamizi wa ngazi ya juu kwa ajili ya maendeleo bora ya jeshi
2023-07-25 14:44:57| CRI

Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) amesisitiza usimamizi wa ngazi ya juu kwa ajili ya kuhimiza maendeleo bora ya jeshi.

Rais Xi amesema hayo jana Jumatatu alipoongoza kikao cha mafunzo ya pamoja cha Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC.

Kikao hicho kiliitishwa kabla ya maadhimisho ya siku ya kuanzishwa kwa Jeshi la Ukombozi la Watu wa China PLA tarehe Mosi, Agosti.