Rais wa China atoa wito wa kujitahidi kutimiza malengo ya uchumi ya mwaka 2023
2023-07-25 08:04:07| CRI

Rais wa China Xi Jinping ametoa wito wa kuongeza juhudi ili kutimiza malengo ya maendeleo ya uchumi ya mwaka 2023.

Akiongoza mkutano na watu wasio wanachama wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kwa lengo la kutafuta mawazo na mapendekezo kuhusu hali ya sasa ya uchumi wa taifa na kazi za uchumi kwa nusu ya pili ya mwaka huu, rais Xi amesema ili kufanya vizuri kazi za uchumi katika kipindi hicho, kanuni ya msingi ya kutafuta maendeleo huku ikihakikisha utulivu inapaswa kuendelea kufuatwa.

Amesema juhudi zinapaswa kuongezwa ili kutekeleza kikamilifu filosofia mpya ya maendeleo katika nyanja zote, kuongeza kasi ya ujenzi wa njia mpya ya maendeleo, kuimarisha kwa kina mageuzi na ufunguaji mlango, kuongeza udhibiti wa jumla, kupanua mahitaji ya ndani, kuongeza kujiamini na kuzuia hatari.

Rais Xi amesema chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China, uchumi wa China umeendelea kufufuka katika nusu ya kwanza ya mwaka, huku mafanikio yakionekana katika maendeleo ya ubora wa juu.