Sekta ya usafiri wa anga ya Kenya yaimarika wakati ukuaji ukichochewa na utalii
2023-07-26 23:18:55| cri

Sekta ya usafiri wa anga ya Kenya imepata pato la shilingi bilioni 78.9 sawa na dola milioni 556 za kimarekani katika nusu ya kwanza ya mwaka huu.

Mkuu wa Shirikisho la mashirika ya utalii la Kenya Bw. Joseph Kithitu amesema mjini Nairobi kuwa sekta ya utalii inafufuka baada ya kudidimia kutokana na maambukizi ya COVID-19, baada ya kuwekwa kwa vizuizi vya utalii vikiwa ni sehemu ya hatua za kukinga na kudhibiti ugonjwa huo.

Mwaka jana Kenya ilipata kipato cha dola milioni 600 hivi kutoka sekta ya usafiri wa anga. Bw. Kithitu amesema wanatarajia kupata dola bilioni 1 za kimarekani katika mwaka 2023 kwa mujibu wa hali ya miezi sita ya kwanza ya mwaka huu, huku akieleza kuwa sekta hiyo inakadiriwa kufufuka kwa pande zote na kurejea katika kiwango cha kabla ya janga la COVID-19 mwaka kesho.

Ameongeza kuwa wageni wengi zaidi hutembelea fukwe na vivutio vya wanyamapori, na utalii wa burudani umekuwa msukumo mkuu kwa ukuaji wa uchumi.