Walinda amani wa China nchini DRC watunukiwa nishani ya amani ya Umoja wa Mataifa
2023-07-26 08:52:39| CRI

Kikundi cha 26 cha walinda amani wa China katika Tume ya ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo jana kilitunukiwa nishani ya amani ya Umoja wa Mataifa.

Hafla ya kutunuku nishani hiyo ilifanyika katika kambi ya uhandisi ya kikundi hicho karibu na mji wa Bukavu, Kivu Kusini.

Kaimu kamanda wa sehemu ya kusini ya tume hiyo Bw. Muhammad Waqar Najeeb amesema walinzi wa amani wa China wamejitolea kikamilifu na kufanya kazi kwa utaalamu, na wametoa mchango mkubwa kwa amani na maendeleo ya sehemu hiyo.