Tanzania kuzalisha dawa za kufubaza makali ya VVU
2023-07-26 14:09:02| cri

Tanzania kwa kushirikiana na kampuni ya VIATRIS itapata fursa ya uwekezaji katika ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha dawa ikiwemo dawa za kufubaza makali ya virusi vya Ukimwi (ARVs).

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya nchini humo, Dk Grace Magembe amesema hayo jana alipofanya mazungumzo na mkurugenzi wa kampuni hiyo wa Kanda ya Afrika, kusini mwa jangwa la Sahara, Prashant Despanande kuhusu fursa za uwekezaji. Naibu Katibu Mkuu huyo amesema uwekezaji wa viwanda vikubwa kama VIATRIS utaiwezesha Tanzania kuwa na upatikanaji wa bidhaa za afya kwa urahisi na kwa gharama nafuu pamoja na kuongeza fursa za ajira kwa watanzania.

Pia amesema, hatua hiyo itaiwezesha Tanzania kuwa na mkakati endelevu katika mwitikio wa mapambano dhidi ya UKIMWI.