Watu 16 wauawa katika mashambulizi nchini Sudan
2023-07-26 14:05:17| cri

Kamati ya Upinzani ya Ombada imesema, watu 16 wameuawa jana jumanne katika mashambulizi ya anga na mizinga katika mji wa Omdurman, magharibi mwa mji mkuu wa Sudan, Khartoum, na kuongeza kuwa, watu wengine wameuawa katika soko la Souk Libya mjini humo.

Wakati huohuo, Umoja wa mataifa umesema hali ya kibinadamu nchini Sudan imegeuka na kuwa janga kamili. Mratibu wa kibinadamu wa Umoja huo nchini Sudan Clementine Nkweta-Salami amesema, mashirika ya kibinadamu yameendelea kutoa huduma kwa watu wa Sudan, huku yakifanya juhudi kubwa kutoa msaada huo katika mazingira magumu.