Rais wa Uturuki akutana na mwanadiplomasia mwandamizi wa China
2023-07-27 08:31:18| CRI

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan jana Julai 26 alikutana na mwanadiplomasia mwandamizi wa China Bw. Wang Yi, kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano wa pande mbili kwenye nyanja mbalimbali.

Rais Erdogan amemtaka Bw. Wang Yi, ambaye ni mkurugenzi wa Ofisi ya Kamisheni ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), kufikisha salamu zake kwa Rais Xi Jinping wa China, akiongeza kuwa Uturuki na China zote ni nchi zenye ushawishi wa kimataifa na umuhimu wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Rais Erdogan amesisitiza kuwa Uturuki itashikilia kanuni ya China-Moja na kusema a nchi yake haiyachukulii maendeleo ya China kama tishio.

Bw. Wang Yi amempongeza Rais Erdogan kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais, na kusema China inaiunga mkono Uturuki kulinda uhuru wa nchi na kutafuta njia ya maendeleo inayoendana na hali halisi ya nchi.