Rais Xi Jinping afanya ziara ya ukaguzi mkoa wa Sichuan
2023-07-27 08:30:29| CRI

Rais Xi Jinping wa China amefanya ziara ya ukaguzi katika mkoa wa Sichuan, kusini magharibi mwa China.

Katika ziara hiyo ya siku mbili kuanzia Jumanne hadi Jumatano, Rais Xi alitembelea sehemu moja ya mfumo wa kale wa barabara unaojulikana kama “Shudao” mjini Guangyuan na kutembelea Jumba la Makumbusho la Sanxingdui mjini Deyang.

Rais Xi amefahamishwa kuhusu juhudi za kuenzi urithi wa kihistoria na kiutamaduni na kulinda mazingira ya asili, maendeleo katika uhamishaji wa wakazi na utafiti kwenye maeneo ya urithi wa kihistoria na kiutamaduni, pamoja na uhifadhi na uchimbaji wa vitu vya kale.