Utafiti uliofanywa nchini Marekani waonyesha ongezeko la Wamarekani wanaounga mkono mgogoro wa kisiasa
2023-07-27 10:40:21| cri

Idadi kubwa ya Wamarekani wanaamini katika matumizi ya mabavu ili kutimiza malengo ya kisiasa.

Hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Chicago cha Marekani na kuchapishwa katika gazeti la The Guardian la nchi hiyo.

Utafiti kuhusu Hatari kwa Demokrasia iliashiria kuwa idadi ya Wamarekani wanaounga mkono matumizi ya mabavu katika siasa inaongezeka wakati kampeni za uchaguzi wa rais utakaofanyika mwakani zikipamba moto.