Bw. Guterres alaani jaribio la mapinduzi nchini Niger
2023-07-27 09:02:48| CRI

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa taarifa kupitia msemaji wake akilaani vikali jaribio la mapinduzi nchini Niger.

Taarifa hiyo imesema Bw. Guterres anafuatilia sana hali nchini Niger, na analaani vikali vitendo vyovyote vya kunyakua madaraka kwa nguvu na kuvuruga utawala wa kidemokrasia, amani na utulivu nchini Niger.

Pia ametoa wito kwa pande husika kujizuia na kuhakikisha zinalinda utaratibu wa katiba. Amesema Umoja wa Mataifa unaiunga mkono serikali na watu wa Niger.