Bibi Peng Liyuan akutana na mke wa rais wa Indonesia
2023-07-28 09:12:37| CRI

Mke wa Rais wa China Bibi Peng Liyuan jana Alhamisi alikutana na Mke wa Rais wa Indonesia Bibi Iriana Joko Widodo huko Chengdu, mji mkuu wa Mkoa wa Sichuan kusini magharibi mwa China.

Bibi Iriana anaambatana na rais Joko Widodo ambaye atahudhuria sherehe za ufunguzi wa Michezo ya 31 ya Vyuo vikuu Duniani ya FISU na kutembelea China.

Bibi Peng Liyuan na Bibi Iriana walitazama kazi za mikono za urithi wa utamaduni usioshikika na maonyesho ya sanaa ya chai.

Bibi Peng amesema China na Indonesia zinafurahia mshikamano wa kitamaduni na uhusiano wa karibu kati ya watu wa nchi hizo mbili, huku akitarajia kuwa pande hizo mbili zitazidisha urafiki kati yao.