Waziri wa TEHAMA wa Kenya akiri kutokea kwa shambulio la udukuzi katika tovuti ya eCitizen
2023-07-28 10:35:46| cri

Waziri wa Habari na Teknolojia ya Mawasiliano (TEHAMA) nchini Kenya Eliud Owalo, amekiri kuwa huduma za serikali kupitia mtandao ziliathiriwa na shambulio katika mtandao, ambalo lilifanywa na watu waliojitambulisha kuwa Watu wasiojulikana wa Sudan.

Hata hivyo, Waziri huyo amesema hakuna data zilizopotea wakati wa shambulio hilo, na kwamba serikali inafanya juhudi kubwa kutatua tatizo hilo na kudhibiti tena jukwaa hilo, na kuongeza kuwa, washambuliaji walianza kwa kufanya tovuti hiyo kufanya kazi kwa kasi ndogo, jambo ambalo amesema linashughulikiwa.

Wananchi wengi wa Kenya wametoa malalamiko yao katika mitandao ya kijamii katika siku nne zilizopita, kuhusu ukosefu wa huduma za serikali kupitia tovuti ya eCitizen.