Mfupa wa mnyama wenye historia ya miaka milioni 20 wagunduliwa nchini Uganda
2023-07-28 10:34:43| cri

Wanasayansi nchini Uganda wamegundua mabaki ya mfupa wa paja wa mnyama mkubwa jamii ya kiboko, unaoaminika kuwa na historia ya miaka karibu milioni 19 mpaka 20.

Mhifadhi Mkuu wa Idara ya Majumba na Minara ya Makumbusho na Mabaki iliyo chini ya Wizara ya Utalii ya Uganda, Sarah Musalizi, amesema mabaki hayo yaligunduliwa katika wilaya ya Napak, kaskazini mwa Uganda siku saba zilizopita, na kuongeza kuwa, wanasayansi walitambua aina ya mnyama kutokana na tafiti zilizochapishwa kuhusu mnyama huyo jamii ya kiboko.

Amesema mkoa wa Karamoja, ambako mabaki hayo yaligunduliwa, ni kame, lakini katika miaka ambayo wanyama hao walikuwa wakiishi, kulikuwa na mito ambayo kwa sasa imetoweka kutokana na mabadiliko ya mazingira.