Rais wa Burundi awasili Chengdu kwa ajili ya Michezo ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Duniani FISU
2023-07-28 14:59:11| cri
Rais Evariste Ndayishimiye wa Burundi Ijumaa aliwasili Chengdu, mji mkuu wa mkoa wa Sichuan, kusini magharibi mwa China, ili kuhudhuria sherehe ya ufunguzi wa Michezo ya 31 ya majira ya joto ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Duniani FISU na kufanya ziara nchini China.