AfDB: Ukuaji wa uchumi wa Afrika Mashariki utaongezeka hadi kufikia asilimia 5.1 mwaka huu
2023-07-28 09:09:07| CRI

Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB imesema ukuaji wa uchumi wa Afrika Mashariki unakadiriwa kuongezeka hadi kufikia asilimia 5.1 mwaka huu kutoka asilimia 4.4 ya mwaka jana.

Kwa mujibu wa ripoti ya “Mtazamo wa Uchumi wa Afrika Mashariki mwaka 2023” inayoonesha tathmini ya AfDB kuhusu hali ya uchumi ya kanda hiyo, makadirio ya muda wa kati na hatari kwa mustakabali wa ukuaji, ufufukaji katika nchi za Afrika Mashariki zilizochaguliwa utachochewa na ufufukaji wa sekta ya huduma na mauzo kwa nje.

Ripoti hiyo pia imechunguza hali ya ukuaji wa kanda hiyo, vichocheo vyake na mustakabali pamoja na athari kwa maendeleo ya uchumi na jamii, ikionesha kuwa kanda ya Afrika Mashariki inakabiliwa na hatari za kushuka za ndani na nje ambazo zinaweza kuathiri ukuaji chanya.