Rais Xi Jinping akutana na mwenzake wa Indonesia
2023-07-28 08:46:59| CRI

Rais Xi Jinping wa China jana Alhamisi alikutana na mwenzake wa Indonesia Joko Widodo mjini Chengdu, mji mkuu wa mkoa wa Sichuan, kusini magharibi mwa China.

Rais Widodo amewasili Chengdu kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa Michezo ya 31 ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Duniani ya FISU na kufanya ziara nchini China.

Kwenye mazungumzo yao, Rais Xi amesema huu ni mwaka wa 10 tangu China na Indonesia zianzishe uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote, na China inapenda kutumia fursa hii kuimarisha ushirikiano wa kimkakati na Indonesia, kuweka mfano wa kuigwa kwa nchi zinazoendelea kukumbatia mustakbali wa pamoja, kutafuta mshikamano na ushirikiano na kuhimiza maendeleo ya pamoja, na pia kuingiza uhakika na nishati chanya kwa kanda na dunia.

Rais Widodo amesema Indonesia inashikilia kithabiti sera ya China Moja na inapenda kuendelea kuimarisha ushirikiano na China kwenye nyanja mbalimbali zikiwemo uwekezaji, uvuvi baharini, usalama wa chakula na huduma za afya.