Rais Vladimir Putin wa Russia amesema nchi yake inatarajia kuimarisha uhusiano na Afrika kwenye nyanja za biashara, uwekezaji na masuala ya kibinadamu ambazo zitafikia mahitaji ya nchi zote.
Rais Putin amesema hayo alipohutubia ufunguzi wa kikao kikuu cha Baraza la Masuala ya Kiuchumi na Kibinadamu kati ya Russia na Afrika, chini ya mfumo wa Mkutano wa pili wa Kilele kati ya Russia na Afrika.
Rais Putin amesema mwaka jana thamani ya biashara kati ya Russia na Afrika ilifikia dola za kimarekani bilioni 18, na anaamini kuwa katika siku zijazo kupitia ushirikiano wa karibu pande hizo mbili zitaweza kuongeza biashara kati yao kwa kiwango kikubwa.
Rais Putin amesema katika mwaka 2022, Russia iliuza tani milioni 11.5 za nafaka kwa Afrika, na karibu tani milioni 10 katika nusu ya kwanza pekee ya mwaka huu, na kwamba itaendelea kutoa nafaka kwa nchi za Afrika.