Rais wa China asema watu wote wanakaribishwa kujionea na kunufaika na maendeleo ya kisasa ya China
2023-07-28 16:56:33| cri

Rais Xi Jinping wa China na mkewe Bibi Peng Liyuan leo asubuhi wameandaa hafla ya kuwakaribisha wageni wa heshima kutoka nchi za nje waliokuja na kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa Michezo ya 31 ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Duniani mjini Chengdu.

Akitoa hotuba kwenye hafla hiyo, rais Xi Jinping amewakaribisha wageni wote kujionea na kunufaika kwa pamoja na maendeleo ya kisasa ya China.

Rais Xi amewataka vijana kote duniani kushikamana ili kuboresha amani na maendeleo duniani. Ameeleza matumaini yake kuwa vijana duniani watachukua fursa ya Michezo ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Duniani kuimarisha maelewano na kuingiza chachu mpya katika maendeleo ya binadamu.

Rais Xi pia ametoa wito wa kuboresha mshikamano kupitia michezo ili kupanga nguvu chanya kwa ajili ya dunia kukabiliana na changamoto mbalimbali na kujenga siku nzuri za baadaye kupitia ushirikiano.

Katika hotuba yake, rais Xi amesisitiza umuhimu wa kuimarisha mawasiliano na kufunzana, na kuboresha maadili ya pamoja ya binadamu na kujenga jamii ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.